Vyama vidogo vya upinzani vimeibua hoja nyingine ya kutokubaliana na mapendekezo ya baraza la wawakilishi ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa mara baada ya kutangazwa matokeo ya kura ya maoni.

Wakizungumza na Zenji Fm wawakilishi wa vyama hivyo kutoka NLD na APPT-MAENDELEO wamesema mfumo huo uliopendekeza utavihusisha vyama vya CCM na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa bila ya kuhusisha makundi mengine.

Naibu katibu mkuu wa NLD, Zanzibar Rashid Ahmmed Joy amesema serikali ya umoja wa kitaifa ni ile inayoshirikisha makundi ya kijamii zikiwemo taasisi za kidini, mabaraza ya wazee, vijana, walemavu na taasisi nyingine.

Amesema endapo mfumo huo wa serikali ya kitaifa utapitishwa na kuvishirikisha vyama vya siasa pekee, chama chake kitangalia uwezekano wa kisheria wa kuzuwia undwaji wa serikali hiyo

Nae mwenyekiti wa baraza la wazee wa chama cha APPT-MAENDELEO, Rashid Yussuf Mchenga amesema chama chake hakikubaliani na mfumo huo kwa vile serikali hiyo itavishirikisha vyama vya CCM na CUF.

Amesema serikali hiyo haitakuwa ya umoja wa kitaifa na badala yake ni serikali ya mseto  ya vyama viwili ambavyo vinaweza kutafautiana katika kuendesha serikali….

Baadhi ya wananchi wengine waliohojia na mwandishi wetu juu ya matokeo hayo ya kura ya maioni wamepongeza kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa itakayondoa migogoro ya kisiasa

Advertisements