Suleiman Kova

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 17 wa ujambazi, silaha tisa, risasi mia moja na 83 na meno ya ndovu manne katika msako uliofanywa katika maeneo mbali mbali mkoani humo.

Kamanda wa polisi wa kanda malum mjini Dar es Salaam Suleiman Kova amewambia waandishi wa habari watuhumiwa hao walikamatwa na polisi baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.

Amesema kumemekuwa na mafaniki makubwa ya kupambana na wahalifu katika mji wa Dar es salaam ikiwa ni pamoja na kuwakamata majambazi sugu ambao walikuwa na uwezo wa kutengeneza risasi.

Advertisements