Sheikh Fadhil Soraga

Viongozi wa dini ya nchini wametakiwa kuungana na kufikia maridhiano ili kuwawezesha wafuasi wa dini hiyo kufunga ibada ya mwezi mtukufu wa ramadhani siku moja na kufungua siku moja.

Katibu wa mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga amesema ni mategemeo ya afisi hiyo hakutakuwa na muumini atakaejitokeza kuwafarakisha waislamu na kugombana katika siku ya kuandama mwezi.

Hata hivyo Sheikh Soraga amesema mwezi wa ramadhani unatarajiwa kuzaliwa siku ya Jumanne na kuandama Jumatano ambapo siku ya kufunga ni Alhamis

Na huko nchini Kenya, Kaimu Kadhi Mkuu Sheikh Ahmad Muhdhar ametoa wito kwa Waislamu nchin kuungana katika kipindi hiki cha kukaribia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Amesema baadhi ya Waislamu huanza saumu bila kusubiri tangazo rasmi la Kadhi Mkuu bali huanza kwa kutegemea mwezi mwandamo katika nchi nyingine.

Amesema tokea jadi Waislamu wa Afrika Mashariki wamekuwa wakianza kufunga na kusherehekea Eid ul Fitr pamoja.

Advertisements