Ujumbe wa wataalamu watano kutoka Jamhuri ya Korea umewasili nchini kuanza kazi za upembuzi yakinifu ya miradi ya kilimo cha umwagiliaji maji.

Wataalamu hao wakiwa nchini watatembelea mabonde ya mpunga ili kuangalia uwezekano wa kiufundi na gharama zitakazohitajika za kuweka miundombinu ya kilimo hicho.

Jumla ya hekta elfu nane 121 Unguja na Pemba zimeanishwa kufanyiwa tathimini hiyo.

Tathimini hiyo pia inatarajiwa kuwashirikisha wataalamu wazalendo wa Zanzibar.

Advertisements