Idara ya kupambana na dawa za kulevya Zanzibar  imesema Zanzibar bado inakabiliwa na ongezeko kubwa la watumiaji wa dawa za kulevya waliokwisha ambukizwa virusi vya ukimwi.

Akizungumza na zenji Fm radio afisa kutoka idara hiyo Kassim Ali Simai amesema asilmia 60 ya watu wanaotumia dawa za kulevya Zanzibar tayari wameshaambukizwa virusi vya Ukimwi.

Amesema hali hiyo ni hatari kutokana na kasi ya maambukizi kwa njia ya kudungana sindano kwa kupitishia dawa ya kulevya ni kubwa ikilinganisha na njia nyingine za maambukizi kama vile kujamiiana kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Simai amesema maeneo yanayoongoza kuwepo kwa watumiaji dawa za kulevya ni Miembeni, Kwahani na Mikunguni.

Hivyo amewataka vijana kutojishirikisha na makundi yasiyo na muelekeo ili kuipunguzia gharama serikali kutokana na kuchukua muda kushuhulikia matibabu ya watu hao.

Advertisements