Rais Aman Abeid Karume

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume ametia saini muswada wa sheria wa marekebisho ya kumi ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 yenye lengo la kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Akizungumza na Zenji fm radio katibu wa baraza la wawakilishi Ibrihim Mzee Ibrahim amesema muswada huo uliopitishwa na baraza la wawakilishi tarehe tisa mwezi huu yametiwa saini na rais Augus 13.

Amesema marekebisho hayo tayari yameshaingizwa katika katiba ya Zanzibar kuanzia tarehe 13 mwezi huu na kinachosubiriwa ni kutolewa kwa nakala mpya ya katiba …

Hata hivyo Ibrahim amesema mfumo wa undwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa umeshatandikwa na kinachosubiriwa ni nia njema na kuaminiana kwa wanasiasa juu ya utekelezaji wa serikali hiyo.

Advertisements