Kassim Ali

Tume ya uchaguzi Zanzibar imesema kampeni za uchaguzi mkuu zilizoanza kwa wagombea wa urais wa jamhuri ya muungano Tanzania, ubunge na udiwani hazitaathiri kampeni za uchaguzi mkuu wa Zanzibar.

Mkurugenzi wa tume hiyo Salum Kassim amesema kampeni hizo kwa wazanzibari hawana tatizo nazo, licha ya baadhi ya wabunge wanaohusika na kampeni hizo wapo hapa Zanzibar.

Amesema kampeni za uchaguzi wa urais, uwakilishi na udiwani kwa ajili ya uchaguzi mkuu  wa Zanzibar zinatarajiwa kuanza Septemba 10 mkwa huu na kumalizika Octoba 30 siku moja kabla ya kupiga kura.

Jana vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi wa urais wa Jamhuri ya muungano Tanzania, ubunge na udiwani vimeanza rasmi kampeni zake kwa wagombea wao.

Advertisements