Madini ya Tanzanite

Tanzanite imepanda bei duniani  kutokana na  kuimarika kwa hali ya uchumi duniani.

Habari zaidi zinasema Tanzanite ambayo haijatengenezwa na yenye rangi nzuri inauzwa kwa dola za kimarikani 166 kwa gram, lakini mwaka uliopita katika kipindi kama hicho, bei ilikuwa dola za kimarekani 128 kwa gram.

Bei ya sasa ya Tanzanite zinazotengenezwa na zenye rangi nzuri ni dola za kimarekani 187 kiasi ambacho ni cha juu sana kuliko bei ya dola za kimarekani 135 ya mwaka uliopita.

Afisa mmoja wa shirika la madini Tanzania amesema biashara ya Tanzanite zinazotengenezwa inatazamiwa kuonesha mafanikio makubwa kama kipindi cha miaka ya tisini.

Inakadiriwa kuwa kufikia mwishoni mwa mwaka huu, soko la Tanzanite litakuwa katika hali nzuri.

Advertisements