Hamad Masauni akisalimiana na rais Kikwete

Wagombea watatu wa ubunge katika majimbo ya mkoa wa mjini magharibi wameekewa pingamizi kwa madai ya kutotimiza masharti katika fomu zao za kuomba kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu.

Msimamizi wa uchaguzi wilaya ya mjini Mashavu Saidi amesema mgombea wa CCM jimbo la Kikwajuni Hamad Yussuf Masauni amewekewa pingamizi na Dr. Idarus Habib Mohammed wa chama cha CUF kwa madai ya kuhushi tarehe yake ya kuzaliwa katika fomu yake.

Amedai katika maelezo yake Masauni amezaliwa Octoba tatu 1979 wakati aliemuweka pingamizi amedai amezaliwa Octoba tatu 1973.

Baada ya mweka pingamizi kushindwa kuthibitisha juu ya madai yake imeamuliwa muweka pingamizi akate rufaa baada ya kushindwa kukubaliana na mkuu wa kituo hicho Mashavu Saidi.

Katika jimbo la Mpendae mgombea mwengine wa CCM Salum Turk amewekewa pingamizi na mgombea wa chama cha jahazi asilia Hassan Mohammed Hamad kwa tuhuma za rushwa.

Muweka pingamizi huyo alitakiwa kupeleka ushahidi ili kuthibitisha madai yake hayo ya rushwa.

Na huko wilaya ya magharibi mgombea mwengine wa CCM Ussi Khamis wa jimbo la Mtoni amewekewa pingamizi na mgombe wa CHADEMA hata hivyo pingamizi hiyo imekatiwa rufaa.

Advertisements