Wafanyakazi wapatao 100 waliokuwa watumishi wa banki ya watu wa Zanzibar PBZ wamelalamikia benki hiyo kutopewa baadhi ya mafao yao tokea kupunguzwa kazini mwaka 2006.

Wakizungumza na Zenji Fm radio wafanyakazi hao wamesema mafao wanayodai ni yale ya kutolewa kazini kabla ya umri wao wa kustaafu licha ya kufungua kesi mahakamani na kushinda kesi hizo.

Mmoja wa wafanyakazi hao wa zamani wa PBZ Salma Salim Omar amesema licha ya kesi hizo kukatiwa rufaa na benki hiyo, madai yao ni kutofuatwa sheria za kupunguza kazini….

Aidha wafanyakazi hao wa zamani wamesema mafao waliolipwa ni kidogo kilichokuwa kati ya shilingi milioni tano hadi mbili, wakati walitegemea kunzia shilingi milioni 20.

Wafanyakazi hao walipunguzwa kwa amri ya serikali kutokana na benki hiyo kuingia katika soko la ushindani wa biashara lililolenga kuwa na wafanyakazi wenye viwango vya elimu ya juu na taaluma

Advertisements