Marehemu Omar Ali Jadi

Wagombea wawili katika uchaguzi mkuu ujao wa nafasi za uwakilishi na udiwani kupitia chama cha wananchi CUF wamefariki dunia usiku wa kumkia leo.

Akizungumza na Zenji fm radio mkurugenzi wa mawasiliano ya umma  CUF Salum Bimani amesema waliofariki ni mgombea wa nafasi ya uwakilishi jimbo la Kojani Omar Ali Jadi.

Amesema Jadi ambae ni mwakilishi wa zamani wa Jimbo hilo amefariki dunia katika hospitali ya Chakechake Pemba

Bimani amemtaja mgombea mwengine aliefariki dunia katika nafasi ya udiwani wadi ya Kikwajuni ni Shani Ahmad Shani.

Amesema mgombea huyo amefariki dunia kwa ajali ya gari alipokuwa akirejesha fomu za kugombea nafasi hiyo.

Bimani ameiambia Zenji Fm radio kuwa CUF inawasiliana na tume ya uchaguzi Zanzibar ili kupeleka majina mengine ya wanachama wao watakaogombea nafasi hizo

Advertisements