Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dr. Ali Mohammed Shein amesema serikali yake itaendelea kuimarisha miundo mbinu ya kiuchumi kisiwani Pemba ili kuwainua kiuchumi wananchi wa kisiwa hicho endapo atapata ridhaa ya kuiongoza Zanzibar.

Amesema wawekezaji kutoka nje ya nchi na wale wazalengo wanaokeza nchi za kigeni wameonesha nia ya kuja kuwekeza Zanzibar hasa maeneo ya Pemba kutokana na kuwepo vivutio vya kiuchumi kama vile umeme wa uhakika, maji na miundo mbunu ya usafirishaji.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu kwa chama hicho kisiwani Pemba Dr. Shein amesema endapo wananchi watamchagua serikali yake itaandaa sera maulum za kuendeleza uchumi kisiwani Pemba kupitia ilani ya uchaguzi.

Amefahamisha kuwa usalama, amani na utulivu wa wananchi utaisaidia Zanzibar kuendeleza sekta za uwekezaji kwa kuwashajihisha wawekezaji wazalendo wanaowekeza nchi za nje pamoja na wawekezaji wageni kuja kuwekeza nchini...

Kuhusu utumishi wa umma Dr. Sheina amesema endapo ataingia madarakani serikali yake itaangalia maslahi ya wafanyakazi kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na mfupi, nyenzo, na kuongeza na mslahi yao.

Amesema wafanyakazi ndio kiini cha mapinduzi ya Zanzibar, hivyo wanahitaji kuendelezwa kwa kupewa taaluma ya kuwatumikia wananchi kwa ufanisi badala ya kubahatisha ili kuliletea tija taifa lao.

Nae mgombea mwenza Dr. Mohammed Gharib amewataka wana CCM kisiwani Pemba kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu ili kuhakikisha chama hicho kinaleta ushindi kwa wagombea wake.

Amesema CCM imejipanga kutekeleza ilani yake ya uchaguzi iwapo kitarudi tena madarakani……

Uzinduzi wa mkutano wa kampeni hizo kisiwani Pemba ulifanyika katika uwanja wa Gombani ya Kale na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi wa mikoa miwili ya Pemba.

Advertisements