Ndege ndogo imeanguka katika kijiji cha Mtende wilaya ya kusini ikiwa na watu wawili.

Akizungumza na Zenji Fm radio kamanda wa polisi wa mkoa wa Kusini Unguja Agostino Oromi amesema ndege hiyo aina ya PA-2.8 ni mali ya kampuni ya Tropical Line School ya  Zanzibar.

Amesema ndege hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na raia wa Iran Teyad Fahad mkaazi wa Chukwani alikuwa na mwanafunzi wake Abrahman Mohammed mkaazi wa Malindi walianguka katika eneo hilo walipokuwa wakifundishana……

Hata hivyo amesema hali za watu hao ni nzuri na wamehojiwa katika kituo cha polisi bila ya kuonekana na majeraha.

Ndege hiyo imepata uharibifu mkubwa katika sehemu za mbele, mabawa na magurudumu

Advertisements