Baadhi ya wagombea wa nafasi za ubunge na uwakilishi katika majimbo ya Pemba wameshindwa kufanya mikutano yao ya kampeni za uchaguzi kutokana na ukosefu wa fedha.

Wagombea hao pia wameshindwa kulipia gharama za fomu ya ubunge yenye thamani ya shilingi elfu 50, fomu ya uwakilishi shilingi laki mbili pamoja na gharama za kuandaa mikutano ya kampeni.

Wakizungumza na mwandishi wetu kiswani Pemba wagombea hao wameilaumu afisi ya msajili wa vyma vya siasa kwa kushindwa kutoa ruzuku kwa vyama vyote vya siasa ili vinadi sera zao sawa na vyama vingine vinavyopata ruzuku.

Miongoni mwa wagombea walioshindwa kufanya mikutano ya kampeni kutokana na ukosefu wa fedha ni mgombea ubunge jimbo la Ziwani kupiita NLD Masoud Ali Nassor

Wagombea wengi wa vyama vya upinzani kwa nafasi za uwakilishi, ubunge na udiwani wameshindwa kunadi sera zao kutokana na ukosefu wa fedha huku wagombea wa vyama vya CCM na CUF vinavyopata ruzuku vikiendelea kufanya mikutano ya kampeni kila jimbo.

Advertisements