Rais Karume akikabidhi Shahada kwa wahitimu wa fani ya ualimu

 

Chama cha wananchi CUF kimewataka wanafunzi waliomaliza mafunzo ya ualimu Zanzibar kujitayarisha kwa ajili ya kupatiwa ajira endapo chama hicho kitapata ridhaa ya kuongoza Zanzibar.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni huko Gombani ya Kale Pemba mgombea urais wa Zanzibar kupitia CUF Seif Sharrif Hamad amedai hakuna sababu ya wahitimu hao kukaa mitaani na taaluma yao wakati skuli zikikabiliwa na uhaba wa waalimu.

Amesema endapo atapta fursa ya kuingia Ikului serikali yake itaendelea kuimarisha sekta ya elimu kwa kujenga vyuo vya ufundi katika mikoa yote ili kuwapatia vijana taaluma ya ufundi ya kujiajiri.

Advertisements