Baraza kuu la wanawake wa kiislamu Tanzania kanda ya wilaya ya magharib limeviomba vyama vya siasa kuacha tabia ya kuchanganya usomaji wa kur-an, dua na ngomba katika mikutano yao ya kampeni.

Barua ya baraza hilo iliyotolewa kwa vyama vya siasa imesema usomaji wa Qur-ani, dua na baadae kufuatiwa na ngomba katika mikutano ya kampeni ni kwenda kinyume na maamrisho ya dini ya kislamu.

Msimamizi mkuu wa baraza hilo Sheikh Abdalla Mnubi Abdalla amesema wakati wa usomaji wa Qur-ani watu wanatakiwa wavae mavazi ya stara, lakini kinachoonekana ni tofauti na maelekezo hayo hasa kwa wanawake.

Hivyo Sheikh Mnubi amewataka viongozi wa vyama vya siasa wanaoshughulikia mikutano ya kampeni kuzuwia usomaji wa Qur-ani katika mikutano ya kampeni inayoendelea nchini kote

Baraza hilo limepeleka barua hiyo ya kutaka kusitishwa kwa usomaji wa Qur-ani na dua katika mikutano ya kampeni za uchaguzi inayoendelea kwa makatibu wa vyama vyote vya siasa viliopo Zanzibar

Advertisements