Maadhimisho kumbukumu ya miaka kumi na moja tangu kutokea kifo cha baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere yanafanyika jioni hii mkoani Kigomba.

Maadhimisho hayo yanayokwenda sambamba na siku ya kuhitimisha mbio za mwengu wa uhuru yanahudhuriwa na viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na serikali ambapo rais Kikwete anawaongoza watanzania katika kumbukumbu hiyo.

Awali maadhimisho hayo yalitanguliwa na ibada ya taifa ya kumuombea dua baba wa taifa katika kanisa Katholic mjini Kigomba.

Katika uhai wake baba wa taifa aliwaonya watanzania kuwa macho na mataifa ya kigeni yanayotumia umasikini wa taifa lao kutaka kuwapokonya mmlaka ya nchi yao

Viongozi mbali mbali wakizungumza za Zenji Fm radio wamemuelezea baba wa taifa ni kiongozi shupavu aliweza kuwaunganisha watanzania wote na kuwa kitu kimoja bila ya kujali dini, ukabila na rangi.

Akizungumza na Zenji fm radio waziri anaeshughulikia masuala ya Muungano Mohammed Seif Khatib amewataka wanzanzibari kuzitumia fursa ziliopo katika kujiendeleza kiuchumi na kielimu..

Advertisements