Jeshi la polisi mkoa wa kaskazini Unguja limezuwia tena mkutano wa kampeni wa chama cha wananchi CUF utakaofanyika kesho katika skuli ya Donge kutokana na kukosekana idhini ya wamiliki wa eneo hilo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa kaskazini Unguja Mselem Masoud Mtulia amesema katika kikao kilichofanyika jana imekubaliwa mkutano huo usifanyika katika uwanja wa skuli ya Donge na badala yake ufanyike katika kiwanja cha Mwanakombo.

Amesema uwamuzi huo hautachukuliwa kwa chama cha CUF pekee bali kwa mikutano yote ya vyama vya siasa kutokana na eneo hilo lipo karibu na hospitali ya kulazia wagonjwa.

Kamanda Mtulia amezitaja sababu nyingine za kutofanyika kwa kwa mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa ni kuendelea kwa mitiahani ya taifa ya kidatu cha nne, kuwepo karibu na msikiti pamoja na uwanja huo hauwezi kuchukua idadi kubwa ya watu.

 

Kutokana na hali hiyo kamanda Mtulia amewataka viongozi wa CUF kutumia busara na kukubaliana na uwamuzi huo kwa vile endapo mkutano huo utaruhusiwa unaweza kuhatarisha uvunjifu wa amani na utulivu.

Nae meneja wa kampeni wa CUF Issa Kheir bada ya kuandaliwa kwa ratiba ya mikutano katia ya vyama vya siasa, tume ya uchaguzi na makamanda wa polisi wa mikoa wamekubaliana vyama hivyo kufanya mikutano kwa mujibu wa ratiba ambayo kiwacha cha skuli ya Donge kimo katika ratiba hiyo……

Advertisements