Mgogoro umejitokeza kati ya waumini wa dini ya kikiristo na kiiislamu katika eneo la Maungani wilaya ya magharibi kwa madai ya kuwepo karibu karibu kanisa na msikiti na kusababisha muingiliano wa ibada.

Mgogoro huo umejitokeza baada ya waumuni wa kikristo kujenga karibu nyumba yao ya kufanyia ibada karibu msikiti.

Akizungumza na zeji fm redio mwenyekiti wa msikiti huo Khalifa Juma Ramadhani amesema wanapofanya ibada, waumini wa dini ya kikiristo hupandisha sauti zao na nyimbo hali inayosababisha mchanganyiko wa sauti za ibada.

Amesema hatua mbalimbali zimechukuliwa kudhibiti tatizo hilo lakini bado limekua likiendelea hadi sasa, hivyo amesema wako katika matayarisho ya kupeleka shauri lao mahakamani

Aidha amesema, kiwanja hicho kilichojengwa kanisa awali kilipangiwa kujengwa skuli ya watoto wadogo pamoja na zahanati, lakini badala yake kumejengwa skuli na kanisa

Nae mwalimu mkuu wa skuli ya All Nation Academy, Kevin Mwagene amesema tatizo hilo halipo bali lipo katika kanisa hilo kwa vile walikubaliana na waumini hao juu ya matumizi ya muda katika kuendesha ibada na masomo yanayoendelea skulini hapo

Advertisements