Jengo la hospitali kuu ya Mnazi mmoja Zanzibar

Rais wa Zanzbiar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume amesema sekta ya afya bado inakabiliwa na ukosefu wa madaktari bingwa na wauguzi wa kuwahudumia wananchi.

Amesema licha ya juhudi zilizochukuliwa na serikali za kujenga vituo vya afya kwa masafa mafupi, lakini bado juhudi zinahitajika ili kuiona Zanzibar inajitegmea kwa kuwa na madaktari bingwa wa kutosha.

Akifungua kituo cha afya katika kijiji cha Kilindi Nungwi kilichojengwa na mmiliki wa hoteli ya kitalii ya Lagema amesema serikali inaendelea kuwasomesha wananchi wake nje na ndani ya nchi ili kupunguza tatizo la madaktari bingwa na wauguzi

Nae waziri wa afya na ustawi wa jamii Sultan Mohammed Mugheir amesema kituo hicho kitatoa matibabu bure kwa wananchi wa vijiji vya mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amesema wizara yake itaendelea kushirikiana na wafadhali wanaojitokeza kusaidia sekta ya afya nchini.

Kituo hicho kilichojengwa na Taasisi ya Reneldo Fondation kimegharimu zaidi ya dola za Marekani laki mbili na elfu 50.

Advertisements