Archive for November, 2010

BENKI YA DUNIA IMESEMA UWEKEZAJI BADO MDOGO TANZANIA

Uwekezaji katika sekta za afya, elimu, kilimo na mazingira nchini Tanzania bado ni mdogo ikilinganishwa na mahitaji ya ukuwaji wa uchumi kupitia sekta hizo.

Taarifa iliyotolewa na benki ya dunia katika mkutano wa ushauriano ulifanyika mjini Zanzibar imesema uwekezaji wa sekta hizo usiozidi asilimia 12 ni mdogo katika utekelezaji wa mipango ya kupunguza umasikini kwa wananchi.

Mwakilishi wa benki hiyo Tanzania bi Chew amesema jumla ya miradi kumi yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.8 imewekeza katika kipindi cha mwaka 2010 kutoka miradi kama hiyo yenye thamani ya dola bilioni 1.6 iliyoekezwa kuanzia mwaka 2007.

Amesema kwa upande wa Zanzibar benki ya dunia imetekeleza maradi wa elimu ya msingi wenye thamani ya dola za Marekani milioni 42 kuanzia mwaka 2007 pamoja na miradi ya MACEMP na TASAF II.

Chew amesema katika kipindi cha mwaka 2011 benki ya dunia itaongeza ufadhili wake kwa Zanzibar katika utekelezaji wa miradi ya utowaji wa huduma mijini wenye thamani wa dola za Marekani milioni 38.

Nao washiriki wa mkutano huo wameiomba benki ya dunia kusaidia mpango wa kuimarisha uchumi na kupunguza umasikini Zanzibar MKUZA hasa katika kilimo cha umwagiliaji maji.

Wamesema sekta ya kilimo ni muajiri mkubwa kwa wananchi, lakini imekosa uwekezaji mkubwa kutokana na wakulima wengi kutomudu gharama za uendeshaji wa kilimo.

Aidha washiriki hao wameishauri benki hiyo kuangalia uwezekano wa kuwasaidia watu wenye ulemavu ambalo ndio waathirika zaidi na umasikini.

Mkutano huo wa siku moja uliofanyika katika hoteli ya Ocean View umewashirikisha wakuu wa taasisi za serikali, jumuiya za kiraia na wandishi wa habari.

SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA KUPUNGUZA UMASIKINI ZANZIBAR

Makamo wa kwanza wa rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema serikali ya umoja wa kitaifa itatekeleza ahadi zake ilizozitoa kwa wananchi za kuwaletea maendeleo na kupunguza umasikini unaowakabili.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara kisiwani Pemba amesema yeye na viongozi wenzake wa ngazi za juu akiwemo rais Shein wanafanyakazi kwa ushirikiano mkubwa ili kutimizia kiu ya maendeleo ya wananchi.

Maalim Hamad ambae pia ni katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF amesema umoja na mshikamano wa ndio utakaoleta mabadiliko ya kuiendeleza Zanzibar kiuchumi.

Hivyo amewataka wananchi wasikubali kurejesha walikotoka katika siasa za chuki na uhasama zilizorejesha maendeleo yao kwa maslahi ya wachache.

Aidha Maalim Hamad aliahidi kusimamia nidhamu na uadilifu kwa viongozi wa serikali ili matarajio ya wananchi yafikiwe kwa vile wamekuwa na matumaini makubwa kwa serikali yao.

Kabla ya mkutano huo wa hadhara mamia ya wananchi mbali mbali Kisiwani Pemba walijitokeza  kumlaki Makamu wa kwanza wa rais, ambaye kwa mara ya kwanza amefanya ziara kisiwani humo tangu kuteuliwa kushika wadhifa huo.                                               17

MAALIM SEIF AWATAKA WAZANZIBARI KUTOKUBALI KUTENGANISHWA

Makamo wa kwanza wa rais Zanzibar Seif Sharif Hamad akiapishwa na rais wa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein Ikulu mjini Zanzibar

Makamo wa kwanza wa rais Zanzibar  Seif Sharif Hamad amewataka wananchi kutowapa nafasi maadui wa Zanzibar wenye lengo la kuwatenganisha baada ya kufikia maridhiano yalioleta amani na utulivu.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa chama hicho huko Kibanda Maiti amesema wananchi wa Zanzibar ni wamoja hivyo hawanabudi kuendeleza na kudumisha eza umoja huo kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.

Maalim Hamad ambae pia nikatibu mkuu wa chama cha wananchi CUFs amesema serikali ya umoja wa kitaifa itatekeleza ahadi zeke ilizozitoa kwa wananchi katika kuwaletea maendeleo

Aidha maalim Seif amemtaka waziri wa biashara kutoruhusu wafanyabiashara kuingiza bidhaa mbovu zinazohatarisha afya za wananchi

RAIS WA ZANZIBAR DR. SHEIN AMEFANYA UTEUZI WA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU WAKE

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa Watendaji Wakuu katika Ofisi na Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Baraza la Mapinduzi na Katibu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Dk Shein amefanya uteuzi huo kutokana na madaraka aliyopewa  chini ya Vifungu 49 (1), 50 (2) na 50 (4)  vya  Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984. Uteuzi huo umeanza leo tarehe 25 Novemba 2010. Walioteuliwa ni

1. BARAZA LA MAPINDUZI 1. KATIBU WA BARAZA LA MAPINDUZI NA KATIBU MKUU KIONGOZI 

DKT. ABDULHAMID YAHYA MZEE

2. NAIBU KATIBU WA BARAZA LA MAPINDUZI

ND. SALMIN AMOUR ABDULLA

 

2. OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, IKULU  

1.     KATIBU MKUU

ND. SALUM MAULID SALUM

2.     NAIBU KATIBU MKUU (IDARA MAALUM ZA SMZ)
ND. ABDULLA JUMA ABDULLA

3.     NAIBU KATIBU MKUU (USHIRIKIANO WA KIMATAIFA NA URATIBU WA SHUGHULI ZA WAZANZIBARI WALIOPO NCHI ZA NJE)
ND. SAID ABDULLA NATEPE

4.     NAIBU KATIBU MKUU (TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA)
ND. MWINYIUSSI ABDULLA HASSAN

 

3. OFISI YA RAIS (FEDHA, UCHUMI NAMIPANGO YA MAENDELEO) 1.       KATIBU MKUU
ND. KHAMIS MUSSA OMAR 

2.       NAIBU KATIBU MKUU (FEDHA)

ND. ABDI KHAMIS FAKI

3.   KATIBU MTENDAJI WA TUME YA     MIPANGO
ND. AMINA KHAMIS SHAABAN

4. OFISI YA RAIS, UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA 

 

1. KATIBU MKUU
ND. JOSEPH ABDULLA MEZA 

2. NAIBU KATIBU MKUU
ND. YAKOUT H. YAKOUT

 

5. OFISI YA MAKAMO WA KWANZA WA RAIS 

 

1. KATIBU MKUU
DR. OMAR D. SHAJAK 

2. NAIBU KATIBU MKUU

DKT. ISLAM SEIF SALUM

 

6. OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS 

 

1.         KATIBU MKUU
DR. KHALID SAID MOHAMED 

2.         NAIBU KATIBU MKUU
ND. SAID SHAABAN SAID

 

7. WIZARA YA KATIBA NA SHERIA 

 

1.         KATIBU MKUU 

ND. ASAA AHMADA RASHID

2.         NAIBU KATIBU MKUU

ND. ABDULGHANI MSOMA

 

8. WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI 

 

1.       KATIBU MKUU 

ND. MWANAID SALEH ABDULLA

2.    NAIBU KATIBU MKUU

ND. ABDULLA MZEE ABDULLA

 

9. WIZARA YA AFYA 1.       KATIBU MKUU 

DR. MOHAMMED SALEH JIDAWI

2.   MKURUGENZI MKUU

DR. MALICK ABDULLA JUMA

 

10. WIZARA YA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO 

 

1.         KATIBU MKUU 

DR. VUAI IDDI LILA

2.         NAIBU KATIBU MKUU

ND. MSANIF HAJI MUSSA

 

11. WIZARA YA USTAWI WA JAMII, NA MAENDELEO YA VIJANA, WANAWAKE NA WATOTO 

 

1.     KATIBU MKUU 

ND. RAHMA MOHAMMED MSHANGAMA

2.     NAIBU KATIBU MKUU

ND. MSHAM ABDULLA KHAMIS

 

12. WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, UTALII NA MICHEZO 

 

1.         KATIBU MKUU 

ND. ALI SALEH MWINYIKAI

2.         NAIBU KATIBU MKUU

ND. ISSA MLINGOTI ALLY

 

13. WIZARA YA ARDHI, MAKAAZI, MAJI NA NISHATI 

 

1.    KATIBU MKUU 

ND.MWALIM A. MWALIM

2.     NAIBU KATIBU MKUU

ND. TAHIR M. K. ABDULLA

 

14. WIZARA YA BIASHARA, VIWANDA NA MASOKO 

 

1.         KATIBU MKUU 

ND. JULIAN RAPHAEL

2.         NAIBU KATIBU MKUU

ND. RASHID ALI SALIM

 

15. WIZARA YA KAZI, UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI NA USHIRIKA 

 

1.         KATIBU MKUU 

ND. ASHA ALI ABDULLA

2.         NAIBU KATIBU MKUU

ND. ALI KHAMIS JUMA

 

16. WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI 1.         KATIBU MKUU 

ND. AFFAN OTHMAN MAALIM

2.         NAIBU KATIBU MKUU (KILIMO)
ND. JUMA ALI JUMA

3.         NAIBU KATIBU MKUU (MALIASILI)

DR. BAKARI S. ASSEID

 

17. WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI 

 

1.         KATIBU MKUU 

DR. KASSIM GHARIB JUMA

2.         NAIBU KATIBU MKUU

DR. OMAR  ALI AMIR

BARAZA LA MAWAZIRI TANZANIA 2010-2015

Rais Jakya Kikwete wa Tanzania akitangaza baraza la mawaziri

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ametangaza baraza lake la mawaziri lenye wizara 26

Orodha ya Baraza la Mawaziri na Manaibu wa Wizara 26 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2010 – 2015

 1. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora – Mathias Chikawe
 2. Waziri wa Nchi, Mahusiano na Uratibu – Steven Wassira
 3. Waziri wa Nchi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma – Hawa Ghasia
 4. Ofisi ya Makamu wa Rais Waziri anayeshughulikia Muungano – Samia Suluhu Hassan
 5. Waziri wa Nchi Mazingira – Dk. Therezia Luoga-Kovisa
 6. Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi wa Sera Uratibu na Bunge – William Lukuvi
 7. Waziri wa Nchi, Uwekezaji na Uwezeshaji – Maria Nagu
 8. Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – George Mkuchika
 9. Naibu Waziri Tawala za Mikoa – Aggrey Mwanri
 10. Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Masuala ya Elimu – Kassim Majaliwa
 11. Waziri Wizara ya Fedha – Mustapha Mkullo
 12. Naibu Waziri Wizara ya Fedha (i) – Gregory Theu
 13. Naibu Waziri Wizara ya Fedha (ii) – Pereira Silima
 14. Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi – Shamsi Vuai Nahodha
 15. Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi – Balozi Khamis Sued Kagasheki
 16. Waziri wa Katiba na Sheria – Selina Kombani
 17. Waziri Wizara ya Mambo ya Nje – Bernard Membe
 18. Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje – Mahadhi Juma Mahadhi
 19. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa – Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi
 20. Waziri Wizara yaMaendeleo ya Mifungo – Dk. Mathayo David Mathayo
 21. Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Mifungo – Benedict Ole Nangoro
 22. Waziri Wizara ya Mawasiliano Sayansi ya Teknolojia –  Profesa Makame Mnyaa M’barawa
 23. Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano Sayansi ya Teknolojia – Charles Kitwanga (almaaruf Mawe Matatu)
 24. Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi – Profesa Anna Kajumulo-Tibaijuka
 25. Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi – Goodluck Ole Medeye
 26. Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii – Ezekiel Maige
 27. Waziri Wizara ya Nishati na Madini – William Mghanga Ngeleja
 28. Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini – Adam Kighoma Ali Malima
 29. Waziri Wizara ya wa Ujenzi (Barabara na Viwanja vya Ndege) – Dk. John Pombe Magufuli
 30. Naibu Waziri Waziri Wizara ya wa Ujenzi – Dk. Harrison Mwakyembe
 31. Waziri Wizara ya Uchukuzi – (Reli, Bandari, Usafiri wa Majini) – Omary Nundu
 32. Naibu Waziri Wizara ya Uchukuzi – Athuman Mfutakamba
 33. Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara -Dk. Cyril Chami
 34. Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara – Lazaro Nyalandu
 35. Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi – Dk. Shukuru Kawambwa
 36. Naibu Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  – Philipo Mulugo
 37. Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii – Dk. Haji Hussein Mpanda
 38. Naibu Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii – Dk. Lucy Nkya
 39. Waziri Wizara ya Kazi na Ajira – Gaudensia Kabaka
 40. Naibu Waziri Wizara ya Kazi na Ajira – Dk. Makongoro Mahanga
 41. Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto – Sophia Simba
 42. Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto – Umi Ali Mwalimu
 43. Waziri Wizara ya Elimu, Habari, Vijana na Michezo – Emmanuel John Nchimbi
 44. Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Habari, Vijana na Michezo – Dk. Fenela Mukangala
 45. Waziri Wizara ya Ushirikiano Afrika Mashariki – Samuel John Sitta
 46. Naibu Waziri  Wizara ya Ushirikiano Afrika Mashariki – Abdallah Juma Abdallah
 47. Waziri Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika – Profesa Jumanne Maghembe
 48. Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika – Christopher Chizza
 49. Waziri Wizara ya Maji – Profesa Mark James Mwandosya
 50. Naibu Waziri Wizara ya Maji – Gerson Lwenge

Tangu aingie madarakani rais Kikwete itakuwa ni mara yake ya tatu kufanya uteuzi wa baraza la mawaziri.

Mwaka 2005 aliunda wizara 29 zenye manaibu 31, kabla ya kulivunja baraza hilo mwaka 2008 na kuunda baraza dogo zaidi likiwa na wizara 26 na lenye manaibu 21

ZANZIBAR YAIOMBA CHINA KUSAIDIA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

Mpunga wa umwagiliaji maji

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeiomba
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuangalia uwezekano wa kusaidia kilimo cha umwagiliaji maji hapa nchini.

Ombi hilo limetolewa na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi alipokutana na Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Li Yiping aliyefika kujitambulisha kwake rasmi.

Balozi Iddi amesema kilimo ni uti wa mgongo wa nchi, hivyo kama kitaendelezwa vizuri kwa kupatiwa nyenzo na wataalamu wa umwagiliaji kinaweza kuimarika na kuimarisha uchumi.

Naye Balozi Li Yiping aliahidi kuendelea kutoa misaada ya maendeleo kwa Zanzibar na kuzidi kuimarisha uhusiano wa nchi mbili hizo.

Wakati huo huo Balozi Iddi alionana na Balozi mdogo wa India aliepo Zanzibar Dalip Sigh Singal, ambapo aliiomba India kusaidia upatikanaji wa matrekta madogo kwa ajili ya wakulima wa Zanzibar.

Naye Balozi Sigh Singal alimpongeza Balozi Iddi kwa kuteuliwa kushika nafasi ya Umakamo wa Pili wa Rais na kueleza matumaini yake kuwa Zanzibar itafaidika sana kwa uzoefu alionao katika uongozi

WAZIRI WA AFYA DUNI AHIDI KULETA MABADILIKO YA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI

Juma Duni Haji

Waziri wa afya na ustawi wa jamii Juma Duni Haji amewataka wananchi kumpa muda wa miezi miwili hadi matatu ili kuleta mabadiliko katika utowaji wa huduma za afya nchini.

Akizungumza na Zenji Fm radio juu la kumaliza tatizo la huduma za afya kwa wananchi amesema wizara ya afya hakuna isomgusa na bado ina matatizo, hivyo atashirikiana na wafanyakazi kuimarisha sekta hiyo.

Aidha waziri Duni sekta ya afya Zanzibar bado inakabiliwa na uhaba wa vifaa vya matibabu, dawa na wataalamu, hivyo amesema atangalia uwezekano kuwaomba watalamu wazalendo walioko nje ya nchi kurejea nyumbani.

Amesema wizara ya afya itafanya mashauriano na wataalamu hao waliokimbia kutokana na maslahi duni na kuahidi kuwaongezea maslahi ili kuja kuwasaidia ndugu zao

Waziri Duni ambae ni kiongozi mwandamizi wa chama cha wananchi CUF ameteuliwa kuwa waziri wa afya kufuatia mfumo mpya wa undaji wa serikali ya umoja wa kitaifa ulioridhiwa na wananchi wa Zanzibar kupitia kura ya maoni.