Chama cha mapinduzi CCM bado kinaendelea kuongoza katika kura za urais wa Zanzibar katika majimbo tisa ya Unguja yaliotangazwa matokeo yake na tume ya uchaguzi Zanzibar kuanzia leo asubuhi.

Akitangaza matokeo hayo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Khatib Mwinyichande amesema mgombea wa CCM Dr. Ali Mohammed Shein ameshinda kwa zaidi ya asilimia 80 katika majimbo ya Donge, Uzini, Chwaka, Muyuni, Mkunduchi, Kitope, wakati jimbo la Koani ameshinda asilimia 69.3, Bumwini asilimia 60.2 na Magomeni asilimia 59.4.

Mgombea wa CUF Seif Sharif Hamad amepata asilimia 10.8 jimbo la Donge, asilimia 17 jimbo la Chwaka na Muyuni, asilimia 29.7 jimbo la Koani, asilimia 15 jimbo la Makunduchi, asilimia 18.4 jimbo la Kitope, asilimia 39.1 jimbo la Bumbwini na asilimia 39.9 jimbo la Magomeni.

Wagombea wengine wa vyama vya AFP, TADEA, NCCR-MAGEUZI, NRA, JAHAZI ASILIA na TADEA wamepata kura chini ya asilimia mbili katika majimbo hayo.

 

Kwa mujibu wa matokeo yaliotolewa na tume ya uchaguzi Zanzibar kuanzia jana usiku mgombea wa CCM Dr. Shein tayari ameshashinda katika majimbo 21 kati ya majimbo 24 ya Unguja yaliotangazwa matokeo.

Nae mgombea wa CUF Seif Sharif Hamad ameshinda kura za urais katika majimbo matatu ya Unguja ambayo ni Mjimkongwe, Magogoni na Mtoni.

Akitangaza baadhi ya matokeo hayo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Khatib Mwinyichande amesema

Huku matokeo hayo yakitangazwa baadhi ya wananchi wamekusanyika nje ya uzio wa mlango wa kuingilia kituo kikuu cha kutangaza matokeo ya urais wa Zanzibar katika hoteli ya Bwawani bila ya kufanya fujo.

Matokeo mengine ya urais katika majimbo ya Pemba yanatarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.

Kwa mara ya kwanza Zanzibar imefanikiwa kuendesha uchaguzi wa mfumo wa vyama vingini kwa amani na utulivu ikilinganishwa na chaguzi tatu zilizopita.                                     28

 

Wakati huo huo Matokeo ya yaliotangazwa muda mfupi uliopita mgombea urais wa Zanzibar kupitia CUF Seif Sharif Hamad ameshinda kura za urais katika majimbo ya Wawi, Chonga, Ole, Chakechake, Mtambwe

Advertisements