Wagombea wa nafasi za uwakilishi na ubunge Zanzibar kupitia chama cha wananchi CUF wanaendelea kushinda katika majimbo mbali mbali kisiwani Pemba.

Matokeo ya hivi karibuni mgombea uwakilishi jimbo la Tumbe kwa tiketi ya CUF Rufai Said Rufai   ameshinda jimbo hilo kwa kupata kura elfu tano 312  na kumshinda mpinzani wake wa karibu wa CCM Amour Khamis Mbarouk aliepata kura 470.

Matokeo ya ubunge jimbo la Mkoani Ali Khamis Seif wa CUF ameshinda jimbo hilo, jimbo la Mkanyageni Mohamed Habib Mnyaa wa CUF ameshinda jimbo la Mtambile mgomea wa CUF Masoud Abdala Salum ameshina ubunge jimbo hilo.

Jimbo la Kiwani mgombea ubunge wa CUF Abdala Haji Ali meshanda wa jimbo hilo, jimbo la Chambani mbunge ni Salum Hemed Khamis wa CUF.   Mwandishi wetu Haji Nassoro kutoka Pemba amesema CLIPS……(SAVED-NASSOR)

Na huko jimbo la Wawi mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CUF Hamad Rashid Mohame ameshinda kwa kupata kura elfu tano 321 na kumshinda mpinzani wake karibu kutoka CCM Daud Khamis Juma aliepata kura elfu mbili 255.

Advertisements