Dr. Shein

Wananchi wa Zanzibar kesho watashudia kitendo cha kihistoria cha kuapishwa rais wa kwanza wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi atakaongoza serikali ya umoja wa kitaifa katika kipindi cha miaka mitano.

Katika sherehe hizo Dr. Ali Mohammed Shein atakula kiapo cha kuiongoza serikali hiyo kufuatia mabadiko ya katiba ya Zanzibar mbele ya umma wa Zanzibar huko katika uwanja wa amani wakati wa asubuhi.

Dr. Shein aliekuwa mgombea urais wa Zanzibar kutoka CCM alitangazwa rais mteule baada ya kupata ushindi wa asilimia 50.1 dhidi ya mpinzani wake wa karibu kutoka CUF Seif Sharif Hamad aliepata asilimia 49.1 ya kura za urais za uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi jana katika hoteli ya Bwawani Dr. Shein ameahidi kuwatumikia wanzanzibari kwa heshima na busara katika mfumo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa.

 

…..2….ZANZIBAR…….

ZANZIBAR……2…….

Hata hivyo amesema serikali ya umoja wa kitaifa bado ni changamoto kwa wazanzibar, lakini ataheshimu maamuzi ya wananchi ya kukubali serikali hiyo ili kuijenga Zanzibar mpya…CLIP…(SAVE-MTEULE).

Wakati huo huo rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume anaemaliza muda wake amewapongeza wananchi wa Zanzibar kwa utulivu na ustahamilivu walionesha wakati wote wa kupiga kura na kutangazwa matokeo.

Amesema ustarabu huo ni ishara ya utamaduni mpya wa siasa unaonesha waafrika wanaweza kuendesha uchaguzi wa amani, utulivu na kufuata sheria.

 

 

Advertisements