Rais Jakaya Kikwete

MGOMBEA wa urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete anaongoza kura za urais katika majimbo 14 ya uchaguzi yaliyokwishatangazwa hadi jana jioni na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Katika majimbo hayo, Rais Kikwete amepata kura 162,439, huku Dk. Willibrod Slaa wa Chadema akipata kura 60,155.

Wagombea wengine akiwamo Profesa Ibrahimu Lipumba wa CUF, amepata 33,819 akifuatiwa na Peter Mziray wa APPT-Maendeleo aliyepata kura 1,806. Hashimu Rungwe wa NCCR-Mageuzi amepata kura 711, Fahmy Dovutwa wa UPDP kura 366 na Mutamwega Mgahywa wa TLP kura 341.

Akitangaza matokeo hayo jana Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Lewis Makame, alitaja majimbo hayo 14 ya awali ambayo matokeo yake yameshafika Tume na kuhakikiwa kuwa ni: Micheweni, Konde, Singida Mjini, Korogwe Mjini, Njombe Kusini, Tumbe, Babati Mjini, Mtwara Mjini na Magogoni.

Mengine ni Bukoba Mjini, Siha, Mpanda Vijijini, Chilonwa na Longido. Singida Mjini, Rais Kikwete anaongoza kwa kupata kura 19,246 akifuatiwa na Dk. Slaa aliyepata kura 5,266. Profesa Lipumba ana kura 922, Mziray kura 93, Mgahywa 24 na Dovutwa kura 22.

Korogwe Mjini Rais Kikwete anaongoza kwa kupata kura 10,761 akifuatiwa na Dk.Slaa mwenye kura 3,135. Profesa Lipumba ana kura 394, Mziray 110, Rungwe 19, Mgahywa tano na Dovutwa sita.

Na katika jimbo la Njombe Kusini, Kikwete ana kura 22,337 na Dk. Slaa 6,848. Mziray ana kura 250, Profesa Lipumba 80, Rungwe 32, Mgahywa 12 na Dovutwa 36, ambapo pia katika jimbo la Mtwara Mjini Kikwete ana kura 18,087.

Profesa Lipumba kura 6,198, Dk. Slaa 4,415, Mgahywa 77, Mziray 161, Rungwe 56 na Dovutwa 33. Longido, Kikwete ana kura 17,067, Dk. Slaa 2,702, Profesa Lipumba 114, Mziray kura 157, Rungwe 10, Mgahywa nne na Dovutwa saba.

Chinolwa, Kikwete ana kura 19,780, Dk. Slaa 2,439, Mziray 319, Lipumba 179, Rungwe 25, Mgahywa na Dovutwa wamefungana kwa kura 18.

Mpanda Vijijini, Kikwete ana kura 7,817, Dk. Slaa 3,669, Lipumba 378, Mziray kura 128, Rungwe 26, Mgahywa kura 17 na Dovutwa 13. Siha, Kikwete ana kura 15,570, Dk.Slaa 7,226, Mziray kura 241, Lipumba 83, Rungwe 18, Dovutwa 14 na Mgahywa kura 11.

Tumbe, Lipumba ana kura 7,021, Kikwete 633, Rungwe kura 127, Slaa 59, Mziray kura 33, Mgahywa kura 36 na Dovutwa 45.

Jaji Makame pia alitangaza matokeo ya jimbo la Micheweni ambapo Profesa Lipumba ana kura 5,674, Kikwete 1,561, Rungwe 168, Dk. Slaa 115, Mgahywa kura 68 na Dovutwa 98. Konde, Lipumba ana kura 6,181, Kikwete 775, Rungwe 66, Slaa 45, Dovutwa 27, Mgahywa 27 na Mziray 20.

Magogoni, Lipumba ana kura 6,044, Kikwete kura 696, Rungwe 79, Dk.Slaa 50, Dovutwa 27, Mgahywa kura 23 na Kuga 22.

Bukoba Mjini, Dk. Slaa kura 16,604, Kikwete kura 15,410, Profesa Lipumba kura 449, Mziray kura 117, Rungwe na Mgahywa wamefungana kwa kura 14 huku Dovutwa akiambulia kura tisa.

Matokeo zaidi ya majimbo mengine yataendelea kutangazwa leo na NEC, kadri itakavyoyapata na kuyahakiki kutoka majimboni.

Advertisements