Dr. Ali Mohammed Shein akila kiapo kuiongoza Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitano 2010-2015

Rais mpya wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein amesema ataunda serikali ya umoja itaifa itakayokidhi mahitaji ya wananchi.

Akizungumza na wananchi mara baada ya kuapishwa katika uwanja wa Amani amesema ili kufanikisha lengo hilo ushirikiano wa wananchi unahitajika katika kuijenga Zanzbiar mpya kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.

Dr. Shein amesema jukumu la urais ni kubwa, lakini atafanya ushauriano na viongozi wa vyama vya siasa, wazee na wananchi wengine katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.

Amesema ushindi alioupata ni wazanzibari wote, hivyo atatumia hekima na busara ili Zanzibar iweze kupata maendeleo na kuwataka wanchi kutodharau na kubeza amani na utulivu iliyopo.

Dr. Shein amesema Zanzibar imekuwa na amani na utulivi ikilinganishwa na miaka mingine

Aidha Dr. Shein amepongeza rais mstaafu Dr. Amani Abeid Karume kwa uongozi wake makini wa kusimamia ilani ya CCM kwa mafanikio makubwa na kuiacha Zanzbiar katika amani.

Amesema mafanikio hayo yamekuwa kichecheo kikubwa kwa wananchi kukiunga mkono chama cha mapindizu na kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo.

Advertisements