Baadhi ya wananchi wamelalamikia mfumuko wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula ikiwemo unga wa ngao, mchele, sukari na mafuta kwa maeneo tofauti ya Zanzibar.

Wakizungumza na ZENJ FM RADIO kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema mfumuko huo wa bei umekuja siku chake tu baada ya kuapishwa kwa rais wa awamu ya saba wa serikali ya mapinduzi Zanzibar.

wamesema kulingana na mfumuko huo wananchi wanashindwa kuelewa tatizo hilo limetokeana na kitu gani hali inayotoa sura mbaya hasa ikizingatiwa ni miongoni mwa vyakula vikuu vinavyotegemewa na wananchi waliowengi hapa Zanzibar.

Akizungumzia juu ya mfumuko wa bei mkurgenzi wa baraza la manispaa Zanzibar Rashid Ali Juma amesema hali hiyo imetokana na upungufu kwa bidhaa ndani ya soko. 

Nae mfanyabiashara wa jumla katika soko la Mwanakwerekwe Alli Salim amesema wao wamepandishwa bei kutokana na bidhaa hizo kupanda kutoka kwa wasambazaji.

Akitaja baadhi ya bidhaa hizo amesema sukari imepanda kutoka shilingi 57 Elfu  kwa kilo hamsini hadi shilingi elfu sitini, unga wa ngano umepanda kutoka  shilingi 40 elfu hadi 50 elfu na mafuta ya kula yamepanda kutoka shilingi 36 hadi  kufikia Elfu 40 kwa katuni.                                  15

Advertisements