Tume ya uchaguzi Zanzibar leo imefanya uteuzi wa wajubme wanawake wa viti maalum 20 watakaoingia katika baraza la wawakilishi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tume ya uchaguzi wajumbe hao wameteuiliwa kufuatia matokeo ya ucahguzi mkuu wa Zanzibar ulifanyika Jupili iliyopita ambapo chama cha CCM kilishinda katika majimbo 28 na CUF ilishinda majimbo 22.

Taarifa hiyo imesema kulingana na uwiano huo CCM imepata nafasi kumi na moja na CUF imepata nafasi tisa za wajumbe wanawake wa viti maalum vya baraza la wawakilishi.

Walioteuliwa kutoka CCM ni Salma Mussa Bilal, Wanu Hafidh Ameir, Mwanaida Kassim Mussa, Amina Idd Mabrouk, Asha Bakar Makame, Mgeni Hassan Juma, Shadya Mohammed Suleiman.

Wengine ni Bihindi Hamad Khamis, Raya Suleiman Hamad, Viwe Khamis Abdala na Panya Ali Abdalla.

Walioteuliwa kutoka CUF ni Zahra Ali Hamad, Ashura Sharif Ali, Asha Abdu Haji, Mtumwa Kheir Mbaraka, Kazija Khamis Kona, Mwajuma Faki Mdachi, Salma Mohammed Ali, Farida Amour Mohammed na Bikame Yussuf Hamad.

Tume ya uchaguzi Zanzibar imesema imefanya uteuzi huo kwa kufuata ibara ya 67 ya katiba ya Zanzibar inayoelezea kutakuwa na wajumbe wa baraza la wawakilishi wanawake kwa idadi ya asilimia 40

Advertisements