Dr. Shein

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein amewateuwa wajumbe wanane wa baraza la wawakilishi.

Walioteuliwa ni Omar Yussuf Mzee, Mohammed Aboud Mohammed, balozi Seif Ali Iddi, Zainab Omar Mohammed na Ramadhan Abdalla Shaaban.

Wengine ni Dr. Sira Ubwa Mwamboya, Juma Duni Haji na Fatma Abdul-habib Fereji.

Dr.  Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 66 cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Uteuzi huo umeanza leo. Wakati huo huo Dr. Shein leo amemuapisha Jaji Omar Othman Makungu kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Hafla hiyo ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Jaji Mkuu wa Zanzibar Hamid Mahmoud

Advertisements