Makamo wa kwanza wa rais wa Zanzibar Seif Sharif Hamad

Makamo wa pili wa arais Zanzibar balozi Seif Ali Idd

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohammed Shein amemteuwa Seif Sharif Hamad kuwa Makamo wa kwanza rais na balozi Seif Ali Idi kuwa makamo wa pili wa rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar .

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyiombo vya habari Dr. Shein amefanya uteuzi huo chini ya vifungu vya 39 vya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Uteuzi huo umeanza leo.

Uteuzi huo uliofanywa na Dr. Shein ni moja ya utekelezaji wa mfumo wa undwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa uliokubaliwa na wananchi kupitia kura ya maoni iliyofanyika hivi karibuni.

Advertisements