Wabunge wa bunge la jamuhuri ya muungano Tanzania leo wamemchagua Anna Semamba Makinda kutoka chama cha CCM kuwa spika wa bunge hilo kwa kipindi cha miaka mitano.

Katibu wa bunge hilo Dr. Thomas Kashililah amesema Makinda amepata kura mia mbili  na 65 na kumshinda mpinzani wake Mabere Nyaucho Marando kutoka CHADEMA alipata kura 53 kati ya kura zote 325.

Makinda anakuwa spika wa kwanza mwanamke wa bunge la jamhuri ya muungano Tanzania kabla na baada ya uhuru.

Advertisements