Makamo wa pili wa rais Balozi Seif Ali Idd

Makamo wa pili wa rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema serikali ya umoja wa kitaifa itahakikisha Zanzibar inapata haki zake zote zinazostahili ndani ya serikali ya jamhuri ya muungano Tanzania.

Amesema nia ya serikali ya awamu ya saba kama ilivyo awamu nyengine ya kudumisha muungano, lakini pia itahakikisha kiwango kikubwa cha kero za muungano zinapatiwa ufumbuzi wa haraka.

Akiahirisha kikao cha baraza la wawakilishi, huko Chukwani Balozi Iddi amesema serikali imekusudia kujenga uchumi imara utakaokuwa msingi wa kuimarisha amani na utulivu iliyopo sasa.

Hivyo amewataka wajumbe wa baraza hilo kushirikiana na serikali katika kujenga maisha bora ya wananchi kwa kuongeza kasi ya uwajibikaji majimboni…….CLIPS…..(SAVED-BALOZI)

Kuhusu uwajibikaji wa serikali Balozi Iddi amesema serikali itaweka nidhamu katika matumizi ya fedha za umma na ukusanyaji wa mapato ili kutimiza kiu ya wazanzibari ya kuwa na maisha bora.

Amesema serikali ya umoja wa kitaifa inakusudia kuijenga Zanzibar mpya yenye mshikamano imara utakaojali maslahi ya jamii badala ya mtu mmoja, vikundi vya watu au vyama vya siasa.

Aidha Balozi Iddi amewataka wajumbe wa baraza la wawakilishi kufanya kazi zao bila ya mivutano na malumbano yasiokuwa ya lazima.

Amesema hatua hiyo haina maana serikali isihojiwe pale inapobidi na kuwataka kufanya kazi kwa nia moja ya kujenga Zanzibar yenye maelewano ya kupigiwa mfano ndani na nje ya Tanzania.

Kikoa cha baraza la wawakilishi kimeahirishwa hadi Januari 19 mwakani.

Advertisements