Majimbo mawili kati ya matatu ya Wilaya ya Magharibi yaliopigiwa kura leo wameshinda wagombea ubunge wa chama cha CUF na jimbo moja kushinda mgombea ubunge wa chama cha CCM.

Majimbo hayo ni Jimbo la Mwanakwerekwe ,Mtoni ,na Magogoni kwa upande wa jimbo la Magogoni waliojiandikisha walikuwa ni 9671 waliopiga kura walikuwa ni 7395 ,kura halali 7301 zilizoharibika zilikuwa 83 ambapo mgombea wa CUF Faki Haji Makame ameshinda kwa 4097,dhidi ya mpinzani wake Usi Amme wa CCM aliyepata kura 2738 Mgombea wa chadema amepata kura 417,mgombea wa tadea kura 9 ,NCCR kura18,TLPkura 8,UDPkura 5,UMD kura 9 UPDP kura 7.

Katika jimbo la Magogoni kura zote zilizopigwa zilikuwa ni 10,155 waliojiandikisha  7556 kura halali 7484 na kura 59 ziliharibika, Mgombea wa CUF Hamadi Ali Hamadi ameshinda kwa kura 4033 dhidi ya mpinzani wake Issa Abeid Mussa aliyepata kura 3264,NRA kura 16,NCCR kura 45,SAU kura 6,Tadea kura17,UMD kura 11.

Uchaguzi wa jimbo la Mwanakwerekwe mgombea wa CCM Haji Juma Sereweji ameibuka mshindi kwa kupata kura 2975 dhidi ya mpinzani wake Usi Juma Hassan wa CUF kwa kupata kura 1971 ambapo waliojiandikisha walikuwa  8,061 kura halali zilikuwa 5083 kura 71 ziliharibika mgombea wa APPT alipata kura 12,Demokrasia makini kura 28,NCCR kura 7,Tadea kura 10,TLP kura 5 na UPDP kura9

Uchaguzi wa Wawabunge umefanyika mara baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo Octoba 31 kulikotokana na upungufu wa karatasi za kupigia kura zilizopokelewa kwa wagombea hao.

 

Advertisements