Ahmed Khalfan Ghailani

Jaji mmoja katika kesi ya kigaidi inayomkabili mtanzania  Ahmed Khalfan Ghailani ameomba kujitoa katika jopo la majaji, hatua inayoangaliwa kama pigo kwa upande wa mashtaka.

Katika risala aliyomtumia Jaji Lewis Kaplan, jaji huyo wa kike, nambari 12, amesema uamuzi wake hauambatani na ule wa wenzake 11 wa jopo la majaji na kwamba anahisi anahujumiwa.

Jaji Kaplan hajazungumza na jaji huyo, na amesema, hata hivyo,  ni mapema mno kuingilia kati wakati majaji wanashauriana.

Jopo la majaji linaendelea na mashauriano na jaji Kaplan amekataa wito wa wawakilishi wa mshtakiwa kutaka kesi ibatilishwe.

Ahmed Khalfan Ghailani, mwenye umri wa miaka 36, Mtanzania anaetokea hapa Zanzibar, anatuhumiwa kuhusika na njama ya mashambulio ya mabomu ya Al Qaida mwaka 1998 katika ofisi za ubalozi wa Marekani nchini Kenya na Tanzania ambapo kiasi ya watu 224 waliuwawa.

Zaidi watuhumiwa 174 ambao bado wanashikiliwa katika kambi ya kijeshi ya Guantanamo, nchini Cuba akiwemo Khalid Sheikh Mohammed anaetuhumiwa kuwa muasisi wa mashambulio ya kigaidi ya september 11 mwaka 2001.

Advertisements