Mizengo Kayanza Peter Pinda

Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania amemteua mbunge wa Katavi mkoani Rukwa, Mizengo Kayanza Peter Pinda, kuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Spika wa bunge Anna Makinda amelitangaza jina hilo siku ya Jumanne 16 Novemba 2010 saa 11 jioni.

Baada ya kusomwa kwa tangazo hilo wabunge wamepiga kura ya kumthibitisha waziri mteule Pinda kwa kupata kura mia mbili na 77  huku kura 49 zimemkataa na kura mbili zimeharibika

Waliowahi kushika nyadhifa za Uwaziri Mkuu tangu Tanganyika kupata Uhuru na hatimaye kuungana na Zanzibar na kuunda Jamhuri ya Tanzania ni:

 1. Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere * (Septemba 2, 1960 – 22 Januari 22, 1962)
 2. Marehemu Rashid Mfaume Kawawa (Januari 22, 1962 – Disemba 1962 )
 3. Marehemu Rashid Mfaume Kawawa (Februari 17, 1972 – Februari 13, 1977)
 4. Marehemu Edward Moringe Sokoine (Februari 13, 1977 – Novemba 7, 1980)
 5. Cleopa David Msuya (Novemba 7, 1980 – Februari 24, 1983)
 6. Marehemu Edward Moringe Sokoine (Februari 24, 1983 – April 12, 1984)
 7. Salim Ahmed Salim (April 24, 1984 – Novemba 5, 1985)
 8. Joseph Sinde Warioba (Novemba 5, 1985 – Novemba 9, 1990)
 9. John Samuel Malecela (Novemba 9, 1990 – Disemba 7, 1994)
 10. Cleopa David Msuya (Disemba 7, 1994 – Novemba 28, 1995)
 11. Frederick Sumaye (Novemba 28, 1995 – Disemba 30, 2005)
 12. Edward Ngoyai Lowassa (Disemba 30, 2005 – Februari 7, 2008
 13. Mizengo Kayanza Peter Pinda (Februari 9, 2008 – Novemba 2010)
 14. Mizengo Kayanza Peter Pinda (Novemba 16, 2010 –


Advertisements