Juma Duni Haji

Waziri wa afya na ustawi wa jamii Juma Duni Haji amewataka wananchi kumpa muda wa miezi miwili hadi matatu ili kuleta mabadiliko katika utowaji wa huduma za afya nchini.

Akizungumza na Zenji Fm radio juu la kumaliza tatizo la huduma za afya kwa wananchi amesema wizara ya afya hakuna isomgusa na bado ina matatizo, hivyo atashirikiana na wafanyakazi kuimarisha sekta hiyo.

Aidha waziri Duni sekta ya afya Zanzibar bado inakabiliwa na uhaba wa vifaa vya matibabu, dawa na wataalamu, hivyo amesema atangalia uwezekano kuwaomba watalamu wazalendo walioko nje ya nchi kurejea nyumbani.

Amesema wizara ya afya itafanya mashauriano na wataalamu hao waliokimbia kutokana na maslahi duni na kuahidi kuwaongezea maslahi ili kuja kuwasaidia ndugu zao

Waziri Duni ambae ni kiongozi mwandamizi wa chama cha wananchi CUF ameteuliwa kuwa waziri wa afya kufuatia mfumo mpya wa undaji wa serikali ya umoja wa kitaifa ulioridhiwa na wananchi wa Zanzibar kupitia kura ya maoni.

 

Advertisements