Makamo wa kwanza wa rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema serikali ya umoja wa kitaifa itatekeleza ahadi zake ilizozitoa kwa wananchi za kuwaletea maendeleo na kupunguza umasikini unaowakabili.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara kisiwani Pemba amesema yeye na viongozi wenzake wa ngazi za juu akiwemo rais Shein wanafanyakazi kwa ushirikiano mkubwa ili kutimizia kiu ya maendeleo ya wananchi.

Maalim Hamad ambae pia ni katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF amesema umoja na mshikamano wa ndio utakaoleta mabadiliko ya kuiendeleza Zanzibar kiuchumi.

Hivyo amewataka wananchi wasikubali kurejesha walikotoka katika siasa za chuki na uhasama zilizorejesha maendeleo yao kwa maslahi ya wachache.

Aidha Maalim Hamad aliahidi kusimamia nidhamu na uadilifu kwa viongozi wa serikali ili matarajio ya wananchi yafikiwe kwa vile wamekuwa na matumaini makubwa kwa serikali yao.

Kabla ya mkutano huo wa hadhara mamia ya wananchi mbali mbali Kisiwani Pemba walijitokeza  kumlaki Makamu wa kwanza wa rais, ambaye kwa mara ya kwanza amefanya ziara kisiwani humo tangu kuteuliwa kushika wadhifa huo.                                               17

Advertisements