Kitabu kitakatifu cha Qur-ani tukufu

Mamia ya waislamu Decemba 2 walihudhuria katika mahakama ya wilaya Mwanakwerekwe kusikiliza kesi  ya mtu aliechoma moto Qur-ani tukufu katika maeneo ya Tomondo wilaya ya magharibi.

Mtuhumiwa huyo  Ibrahi ambae alisilimu na baadae kurudi kwenye ukiristo alichoma moto Qur-ani hiyo Novemba 2010.

Awali kijana huyo alisilimu kwa hiari yake na kupewa nyumba ya kuishi. Mahakama ya Mwanakwerekwe imeahirisha kesi hiyo hadi Decemba 13 mwaka 2010.

Kijana huyo anaedaiwa kuchoma moto Qur-ani hiyo alikuwa na mtindo wa kwenda kanisani na baada ya kuonekana na mwenendo huo muislamu aliempa nyumba yake kwa ajili ya kuishi alimwambia ahame na ndipo mkewe ambae hajasilimu alimshawishi kuichoma moto Qur-ani.

Kitabu hicho kitakatifu kilichomwa moto pamoja na taka zilizosafishwa kwenye nyumba anayoishi Ibrahim katika eneo la Tomondo.

Inasemekana mtoto mmoja aliekuwa akipita njia alikiona kitabu cha Qur-ani kikichomwa moto na kutoa taarifa kwa waisalmu wanaoishi eneo hilo.

Baada ya kupata taarifa hizo waislamu walimkamata Ibrahim na kumpeleka kituo cha polisi cha Mazizini na kufunguliwa kesi katika mahakama ya wilaya Mwanakwerekwe.

Wakizungumzia kesi hiyo baadhi ya walislamu waliohudhuria wamesema iwapo kesi hiyo itazunguushwa hawatavumilia

Advertisements