Profisa Issa Shivji

Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Professa Issa Shivji amesema Zanzibar inahitaji kuandikiwa katiba mpya itakayoendana na mfumo wa sasa wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Amesema licha ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kufanyiwa marekebisho, lakini bado haijitoshelezi kuendeshea serikali ya umoja wa kitaifa iliyokubaliwa na wananchi kupitia kura ya maoni.

Akitoa mada katika kongamano la kitaifa la mjadala wa serikali ya umoja wa kitaifa mjini hapa Profisa Shivji mesema dhana ya upinzani katika serikali hiyo imekufa kutokana na kukosa ukoswaji wa serikali.

Akifungua kongamano hilo Makamu wa pili wa rais, Balozi Seif Ali Iddi amewataka mawaziri kufanya kazi kama mawaziri wa serikali badala ya kuweka mbele maslahi ya vyama vyao vya siasa wanavyotoka.

Marehemu Profisa Haroub Othman

Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar lilikuwa ni miongoni mwa kumbukumbu ya kumuenzi mwanaharakati wa haki za binadamu Marehemu Profisa Haroub Othman

Advertisements