Meli ya Mv maendeleo ikishusha abiria na mizigo katika bandari ya Mkoani Pemba

Abiria kadhaa waliokuwa wasafiri kwa meli ya Mv. Maendeleo kutoka Pemba kwenda Unguja wamekwama katika bandari ya Mkoani baada ya meli hiyo kuzuiliwa kuwasafirisha abiria kutokana na uchakavu.

Waziri wa miundo mbinu Hamad Masoud ameizuwia meli hiyo  kutokana na ubovu na kutembea kwa mashine moja kwa muda mrefu badala ya mashine mbili za kawaida.

Amesema serikali inajali na kuthamini maisha ya wananchi hivyo haiko tayari kuona meli hiyo mbovu inasafirisha abiria kwa kutumia mashine moja ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya wasafiri.

Kabla ya kupigwa marufuku meli hiyo ilidaiwa kuharibika mara mbili ilipokuwa safarini kutoka Unguja kwenda Pemba na kusaidiwa kwa kuvutwa na tagi hadi katika bandari ya Mkoani.

Meli ya Mv  maendeleo inategemewa sana na wananchi wanaosafiri kati ya visiwa vya Unguja na Pemba, hivyo kuharibika kwake kunaweza kuleta usumbufu mkubwa.

Advertisements