Wananchi wa maeneo ya Vitongoji Pemba wameiomba serikali kuwarejeshea maeneo yao ya kilimo na ufugaji yanayodaiwa kuhodhiwa na baadhi ya wafanyabiashara na wanasiasa.

Mmoja wa wananchi wa Vitongoji waliochukuliwa maeneo yao Abdalla Khamis Abdalla ameiyomba serikali kuwarejeshea maeneo yao ili waendelee na shughuli zao za kutafuta maisha katika maeneo hayo.

Amesema endapo serikali itaendelea kuwapuuza wananchi na kuwaachia watu  wachache kuyatumia maeneo hayo kwa maslahi yao kutawanyima wananchi wa Vitongoji maeneo ya kilimo na mifugo wanayoendeshea maisha yao ya kila siku.

Maeneo yanayodaiwa kupewa wafanyabiashara na wanasiasa ni Kibokoni, Kiliko Cheupe ,Liko la Vumba, Makoba na Makaani kwa Ali Ussi huku baadhi ya vigogo wa Serikali wakitajwa kuhusika na umiliki ama kuyagawa maeneo hayo.

Wakati huo huo mwakilishi wa jimbo la Wawi Saleh Nassor Juma ameahidi ameahidi kulifuatilia suala hilo kisheria ili kuhakikisha wananchi wa Vitongoji wanarejeshewa katika maeneo hao kwa kuendeleza shughuli za kilimo na fugaji.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Machomanne Chake Chake amesema eneo hilo linalotumiwa na wananchi kwa shughuli za kiuchumi kama vile kilimo na ufugaji limehodhiwa na baadhi ya wanasiasa akidai hawakufuata utaratibu.

Hivi karibuni makamo wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwagiza watendaji wa serikali wakiwemo masheha waliohusika na uzaji wa ardhi kiholela kufuta nyaraka zote na kurejesha fedha walizouza maeneo ya ardhi.

Advertisements