Notherland Flag

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na serikali ya Netherlands zimetiliana saini mkataba wa Mradi wa kuimarisha afya za mama wajawazito na watoto wenye thamani wa EURO Milioni nane .

Akizungumza mara baada ya utiaji saini huo Katibu mkuu wizara ya nchi afisi ya rais Fedha uchumu na Mipango ya Maendeleo Khamis Mussa Omar amesema kuwa mradi huo pia utaimarisha hospitali 15 za vijijini Unguja na Pemba na kuifanyia matengenezo miundombinu ya maji na umeme katika hospitali hizo.

Mradi huo unatarajiwa kutoa kipaumbele mpango wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini MKUZA na kuendeleza mipango ya Millenium ya kupunguza vifo vitakanavyo na uzazi wa mama na watoto .

Mradi huo wa miaka mitatu ambao fedha zake zitatolewa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Netherlands pia utahusisha ujenzi wa jengo la horofa tatu za wodi ya akinamama na watoto ,kuendesha mafunzo kwa wakunga wa jadi na dawa za asili pamoja na mpango wa usimamizi wa hospitali.

Advertisements