Pandu Ameir Kificho

Spika wa baraza la wawakilishi Pandu ameir Kificho amesema changamoto kubwa inayoikabili serikali ya umoja wa kitaifa ni kuendelea kujifunza katika nchi zinazoendesha mfumo huo duniani.

Amesema  mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa ni mpya hivyo unahitaji umakini wa hali ya juu katika kuendeleza adhma ya umoja  wa wazanzibar.

Spika Kificho ameeleza hayo katika ofisi za baraza la wawakilishi Mbweni alipokuwa na mazungumzo na ujumbe kutoka ubalozi wa Netherlands  nchini Tanzania.

Hata hivyo amezitaka nchi nyengine za Afrika kujifunza mabadiliko ya mfumo wa kisiasa inayotokana na misingi ya ridhaa za wananchi kama ilivyo Zanzibar kwa sasa.

Kuhusu uwezekano wa kuanzishwa kwa mfumo wa aina hiyo Tanzania bara, Kificho amesema itategemea mazingira na haja ya kuwepo kwa mfumo huo hapo baadae.

Naye balozi wa netherland nchini Tanzania Dr. Ad Koekkoek ameipongeza Zanzibar kufikia mabadiliko ya kisiasa na kikatiba.

Hata hivyo ameishauri serikali ya umoja wa kitaifa kuwa makini katika kuhakikisha inafikia matarajio ya watu katikakuwaletea maendeleo.

Awali serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na serikali ya Netherlands zimetiliana saini mkataba wa Mradi wa kuimarisha afya za mama wajawazito na watoto wenye thamani wa EURO Milioni nane .

 

 

Advertisements