Waislamu nchini wameshauriwa kuzingatia utekelezaji wa mikataba ya kimataifa inayodaiwa kutetea haki za binadamu kwa vile inakwenda kinyume na maadili ya dini ya kislamu.

Mwanazuoni wa kislamu kutoka Jamaica Dr. Bilal Phillip akizungumza katika mahojiano na radio Nour amesema mikataba hiyo inayoendelea kutekelezwa ikiwemo ndoa za jinsia moja ni uovu wa maadili katika jamii.

Amesema utetezi wa ndoa za jinsia moja ulionea katika nchi za magharibi unaweza kusababisha maovu mengine ndani ya jamii ikiwemo uzinifu kwa watoto wadogo na uonevu kwa wanawake.

Aidha Dr. Bilal ambae kwa sasa anaishi nchini Qarta amevita vyuo vya kislamu kuendelea kubadilisha umma wa waislamu kwa kutumia elimu ya dini.

Advertisements