Rais mstaafu wa Zanzibar Dr. Amani Karume akiwa na binti yake Fatma Karume akionesha eneo analodaiwa kulipora

Rais mstaafu wa Zanzibar Dr. Amani Abeid Karume amekitaka kituo cha televisheni ya serikali ya mapinduzi Zanzibar TVZ kumuomba radhi baada ya kutoa tarifa zilizomshushia hadhi yake juu ya mgogoro wa ardhi katika eneo la Mbweni.

Amesema taarifa zilizotolewa na kituo hicho zimepotosha ukweli juu ya umiliki wa ardhi wa eneo hilo na kuonekana kwa wananchi amevunja sheria za umiliki wa ardhi.

Akizungumza na waandishi wa habari huko nyumbani kwake Mbweni Dr. Karume amesema kituo hicho kimetumiwa na watu wachache kuwadanganya wananchi na hawezi kukishtaki, lakini amekiomba kumuomba radhi

Akizungumzia mgogoro huo wa ardhi kati ya binti yake Fatma Amani na waumini wa kikiristo wa kanisa na Anglikana Mbweni amesema nyaraka za umiliki wa ardhi zinaonesha eneo analotaka kujenga binti yake limo katika sehemu ya ardhi inayomilikiwa na rais wa kwanza wa Zanziar Abeid Karume.

Amesema eneo hilo limepakana na eneo la kanisa ambalo amesema kutokana na kumbukumbu za nyaraka zinaonesha eneo hilo halimilikiwa na kanisa na miliki halali ni Jumuiya ya wahindi tokea mwaka 1932.

Dr. Karuma amesema baada ya mapinduzi ya mwaka 1964 ardhi yote ya Zanzibar ilitaifisha na kuwa chini ya serikali, lakini baada ya kugaiwa kwa wananchi hakuna hati zinazoonesha eneo hilo linamilikiwa na kanisa.

Nae Fatma ambae anadaiwa kujenga nyumba ya kuishi katika eneo la makaburi amekanusha madai hayo na kuwatupia lawama viongozi wa kanisa hilo kwa kukubali kuharibu makaburi hayo kwa maslahi binafsi.

Amesema eneo la makaburi halijamuhusu na amejenga katika eneo la familia yake

Hivi karibuni waumini wa kanisa hilo wameripotiwa kuharibu ujenzi wa nyuma ya Fatma uliokuwa katika hatua ya msingi kwa kile walichodai kujenga kwenye eneo la makaburi ya wakiristo.

Advertisements