Kikosi cha jeshi la polisi Tanzania cha kutuliza fujo FFU

Polisi ya Tanzania yathibitisha kuwa watu wawili wamekufa baada ya mapambano kati yake na waandamanaji wa chama kikuu cha upinzani nchini humo, Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kwa uchache watu wawili wamekufa baada ya kupigwa risasi na Polisi wa Tanzania katika mji wa Kaskazini wa Arusha na wengine wengi wanashikiliwa na jeshi hilo hadi sasa.

Miongoni mwa waliokamatwa na viongozi 10 wa chama cha CHADEMA, akiwemo aliyekuwa mgombea wa urais wa chama hicho katika uchaguzi uliopita, Dkt. Wilbrod Slaa na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, pamoja na wabunge wa eneo hilo.

Chanzo cha maandamano hayo ni kuupinga uchaguzi wa meya wa Arusha kwa madai kwamba idadi ya madiwani wanaoviwakilisha vyama vya CCM na CHADEMA inafanana ila walizuiwa kupiga kura. Mwandishi wetu wa Arusha, Nicodemus Ikonko, amekifuatilia kisa hicho na hii hapa taarifa yake

Advertisements