Bado mchele unauzwa kwa bei ya juu Zanzibar

Serikali ya mapinduzi Zanzibar inakusudia kuandaa sheria itakayowabana wafanyabishara wanaopandisha bei za bidhaa kiholela.

Akizungumza na Zenji Fm radio waziri wa viwanda, bishara na masoko Nassor Ahmed Mazurui amesema licha ya serikali kupunguza ushuru wa bidhaa, lakini bei za bidhaa bodo ziko juu kwa maslahi binafsi.

Amesema ni kweli bei za bidhaa katika soko la dunia zimepanda, lakini bei zinazouzwa bidhaa hizo nchini hasa za vyakula kama vile mchele, sukari, unga wa ngano ziko juu ikilinganishwa na bei katika soko la dunia.

Amesema wafanyabishara wamekuwa wakitumia mwanya wa kulimbikiza bidhaa zao maghalani na zinapotolewa huuzwa kwa bei ya juu wakati waliponunua bidhaa hizo katika soko la dunia zilikuwa nchini

Waziri  Mazuri amefahamisha kuwa bei ya mchele wa chini katika soko la dunia ni dola 480 ukifika Unguja na dola 610 kwa Pemba, lakini mchele huo huuzwa kwa shilingi elfu 46 kwa kilo 50 bei ambayo amedai ni kubwa

Kauli hiyo ya waziri imekuja huku bei za bidhaa hasa za vyakula zikiwa zimepanda tofauti na matarajio ya wananchi ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Advertisements