Eneo la bandari la Zanzibar

Meli moja ya kitalii  imelazimika kutia nanga kwa dharura katika bandari kuu ya Malindi, mjini Zanzibar baada ya kukosewa kutekwa nayara na maharamia wa kisomalia katika barahi ya Hindi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na maafisa wa banadari hiyo wamesema meli hiyo iliwasili bandarini hapo jana asubuhi ikiwa katika safari za kuwaida na kuondoka jioni ikielekea mjini Dar es Salaam.

Hata hivyo usajili wa meli hiyo pamoja na idadi ya abiria na wafanyakazi  waliokuwemo ndani ya meli hiyo bado haijafahamika na sehemu inayotokea.

Hiyo ni meli ya pili kufika Zanzibar ikijaribu kuwakimbia maharamia wa kisomali wanaotaka kuiteka nyara.

Maharamia wa kisomali wamekuwa tishio katika bahari ya Hindi kwa meli za mizigo na abiria, hali iliyofanya gharama za huduma za usafiri kuongezeka na kuwathiri wananchi wa eneo hilo kutokana na kuongezeka bei za bidhaa.

Advertisements