Mitambo ya kuchimbia mafuta Zanzibar tokea enzi za ukoloni

Chama cha siasa cha wakulima A.F.P kimetaka kuharakishwa kuondolewa kwa raslimali ya mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya muungano.

Akizungumza na zenji fm radio kwa njia ya simu kutoka kisiwani Pemba mwenyekiti wa chama hicho Said Soud amesema hatua hiyo itasaidia  kuzirejesha raslimali hizo mikono mwa wazanzibari kihalali na kuchimwa kwa haraka.

Hata hivyo amesema katiba ya Zanzibar pia inahitaji kufanyiwa mabadiliko mengine ya kumi na moja ili kuanisha mafuta na gesi asilia kuwa sio mambo ya muungano.

Amesema wananchi wa Zanzibar wamekuwa katika dimbwi la umasikini hivyo kuharakishwa kwa uchimbaji wa mafuta utawasaidia kujikwamua kiuchumi

Kauli hiyo ya chama cha A.F.P inakuja sambamba na maoni tofauti ya watanzania wanaopendekeza muundo wa katiba mpya ya Tanzania baada ya rais Kikwete kuonesha nia ya kufanya hivyo.

Advertisements