Taabu ya usafiri Pemba

Wananchi wanaosafiri kwenda kisiwani Pemba kwa usafiri wa baharini wameiomba serikali kuingiliakati uzwaji wa tiketi unaofanywa kwa njia ya magendo.

Akizungumza na Zenji fm radio mmoja wa wananchi hao Omar Abass Omar amesema  tiketi nyingi zimekuwa zikuzwa kwa njia ya magendo kati ya shilingi elfu 15 hadi 20 wakati bei halali ni shilingi elfu kumi kwa meli zinazoondoka usiku.

Amesema  tiketi hizo huuzwa kwa watu wasiohusika na badala yake huziuzwa kwa bei ya juu hivyo ameiomba serikali kuingilia kati suala hilo kwa vile linaleta usumbufu kwa wasafiri

Usafiri wa baharini kisiwani Pemba umekuwa ukileta usumbufu baada ya meli ya Mv. Maendeleo kuzuiliwa kusafirisha abiria kutokana na ubovu ambayo ya kwa sasa iko chelezoni Mombasa

Advertisements